Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ametoa zawadi ya Sikukuu ya Idd kwa watoto 43 wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha SWACCO kilichopo Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Zawadi hizo zimekabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye aliwakilishwa na MKuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema
Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na Michele,sukari ,unga wa ngapi,maharage na mbuzi mawili kwa ajili ya kitoweo.
Diwani wa Kata ya Mwengemshindo Mheshimiwa Osmund Kapinga akizungumza kwenye hafla hiyo amemshukuru Waziri Mkuu kwa zawadi hiyo ya Idi ambayo ameitoa kwa watoto hao yatima na wenye mahitaji maalum.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.