Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro amekamilisha ziara ya kiserikali ya kutembelea kata zote 21 za Manispaa ya Songea.
Lengo kuu la ziara hiyo likiwa ni kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi .
Dkt.Ndumbaro alianza ziara hiyo kuanzia tarehe 09 Julai 2024 na kuhitimisha tarehe 17 Julai 2024.
Katika ziara hiyo Dkt. Ndumbaro aliambatana na Wataalamu mbalimbali kutoka Sekta ya Elimu, Afya, Mipango miji, Uchumi, Kilimo, Tasaf, TARURA, TANROAD, SOUWASA, viongozi wa vyama vya Siasa, na Waheshimiwa Madiwani ambapo amefanikiwa kukamilisha kutembelea kata zote 21 za jimbo la Songea Mjini.
Miongoni mwa kero ambazo amesikiliza na kuzitafutia ufumbuzi ni changamoto ya miundombinu ya Barabara, Vivuko na mifereji, ukamilishaji wa miundominu ya ofisi za Serikali za mita, miundombinu ya elimu Msingi, umeme, na maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.