Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro ametoa wito kwa Wizara, Taasisi za Umma kuitumia Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ili kuondokana na changamoto ya kufanya marekebisho ya sheria mara kwa mara.
Waziri Ndumbaro ametoa wito huo Jijini Dodoma wakati akipokea ripoti maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani January Msoffe alipowasilisha ripoti kuhusu mapitio ya sheria zinazosimamia uchaguzi wa vyama vya siasa nchini na sheria zinazosimamia utoaji haki katika mahakama ya mwanzo.
“Hii itaepusha changamoto ya sheria kufanyiwa marekebisho mara kwa mara kwakuwa tume ina wataalam waliobobea katika tafiti za kisheia hivyo waitumie,” amesema Dk. Ndumbaro na kuongeza kuwa bila kufanya hivyo taarifa zao hazitapokelewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.