Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Filbertho Sanga na wakuu,wa Divisheni,walimu wakuu s/m na wakuu wa shule za Sekondari watendaji wa Kata na maafisa Elimu Kata.amefanya kikao kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Limbo.
Lengo la kikao ni kufanya maandalizi na kuweka mikakati ya kuanza mwaka mpya 2024 katika sekta ya elimu.
Akifungua kikao amewataka wataalam wa elimu kufanya Tathimini ya mwaka uliopita na kumtaka kutatua changamoto zilizojitokeza katika sekta ya elimu na kuweka mikakati ya kuboresha.
Aidha wakati akifunga kikao amewataka washiriki kuhakikisha kuwa,
Miradi ya Maendeleo inasimamiwa na inakamilika Kwa wakati.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato Cha kwanza waripoti mara shule inapofunguliwa na walimu wawapokee watoto bila masharti yoyote.
Wafanyakazi watoe huduma Bora Kwa wananchi na kuwa mfano Bora wa serikali.
Aidha ametoa onyo Kali Kwa wazazi walezi ambao hawatawaketa shule watoto.
Kukomesha mimba Kwa wanafunzi Kwa kuchukua hatua Kali Kwa wahusika.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.