• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BADO jitihada zinahitajika kushughulikia Hoja za CAG

Imewekwa kuanzia tarehe: June 19th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amesema kuwa juhudi za Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa katika kushughulikia hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni za kuridhisha kwa kiasi fulani kwa kuwa bado jitihada zinahitajika katika kutekeleza hoja hizo.

Makondo ametoa kauli hiyo wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed,  katika Baraza Maalum la kujadili hoja za CAG lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

"Pamoja na kupata hati safi, mwenendo wenu wa ushughulikiaji wa hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pamoja na maagizo ya LAAC kwa kiasi fulani unaridhisha, namaanisha bado zipo jitihada ambazo mnapaswa kuzifanyia kazi ili tuweze kufikia hatua nyingine ya kuzimaliza hoja pamoja na maelekezo ya kamati," alisema Makondo.

Amebainisha kuwa kwa mujibu wa ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2024, jumla ya hoja 41 zilitolewa kwa Halmashauri ya Nyasa, kati ya hizo, hoja 24 zimefanyiwa kazi na kufungwa, 17 zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji, pia bado kuna hoja 12 za miaka iliyopita na maagizo matano ya Kamati ya Bunge ya LAAC ambayo hayajatekelezwa ipasavyo.

Makondo amewaagiza wakuu wa idara na vitengo vya halmashauri kushiriki kikamilifu katika kuandaa majibu ya hoja pamoja na mpango kazi wa utekelezaji hoja za CAG, kuandaa taarifa za hesabu za mwisho wa mwaka kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uhasibu katika sekta ya umma, huku akisisitiza kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi watakaobainika kusababisha hoja au hasara kutokana na uzembe.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa, Bw. Salum Ismail, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya Mhe. Peres Magiri, amewapongeza madiwani na menejimenti ya halmashauri, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji kwa kazi nzuri iliyowezesha halmashauri kupata hati safi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw. Khalid Khalif ameahidi kuwa Halmashauri ya Nyasa itaendelea kutekeleza majukumu ya serikali kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozo kwa uadilifu na uwajibikaji wa hali ya juu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • SERIKALI yatoa bilioni 3.4 kumaliza kero ya maji Tunduru

    June 29, 2025
  • KIWANDA kikubwa cha mbolea kitakachowanufaisha wakulima Ruvuma chazinduliwa

    June 29, 2025
  • RAS Ruvuma ateta na viongozi wa NHIF

    June 26, 2025
  • CHACHA amekabidhi ofisi Masanja Tunduru

    June 26, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.