Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 2.5 kupitia mradi wa kuboresha miundombinu ya shule za sekondari (SEQUIP) kwaajili ya ujenzi wa shule 5 za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mwalimu Rudia Elias Masatu, ambapo amesema fedha hizo zimetumika kujenga sekondari 5 ambazo ni Majimaji, Mpakate, Kungu, Tuwe Macho na Tinginya ambazo tayari zina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tatu.
Naye Mwalimu Mkuu wa Kungu sekondari, Ayoub Kundya, amesema walipokea shilingi milioni 480 mwaka 2022 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 8, jengo la utawala, maktaba, chumba cha kompyuta pamoja na maabara tatu za masomo ya Fizikia, Kemia na Biolojia, na shilingi milioni 95 kwaajili ya ujenzi wa nyumba za walimu ambazo zimekamilika, na shule hiyo tayari ina wanafunzi 467 wa kidato cha kwanza hadi cha tatu.
Kwa upande wake mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Kungu sekondari, Frahma Seif Ali, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwaletea shule nzuri na amehaidi wataongeza bidii ili kufanya vizuri kitaaluma.
Kwa upande mwingine Mjumbe wa Bodi ya Kungu sekondari, Mahmoud Selemani, amesema mwanzo wanafunzi walikuwa wanapata shida ya kutembea umbali mrefu hivyo shule hiyo imepunguza adha hiyo na sasa itawasaidia kupata masomo kwa wakati.
Katika hatua nyingine mzazi wa mwanafunzi anyesoma Kungu sekondari, Ahmad Mtumbi, amesema wamepata madarasa mazuri, shule ina muonekano mzuri na yenye mandhari mazuri.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.