CHAMA cha Mapinduzi wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,kimempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Sh.bilioni 145.77 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mwinyi Msolomi,wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Songea mjini baada ya kutembelea mradi wa maji wa miji 28 unaotekelezwa na Mkandarasi kampuni ya China Civil Engineering Contruction Corporation(CCECC).
Mradi huo,unatarajiwa kumaliza kero ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Songea hasa wanaoishi mtaa wa Sokoine kata ya Bombambili na Making’inda kata ya Msamala ambao mara kwa mara wanapata maji kwa mgao.
Msolomi,ameishukuru Serikali kupitia wizara ya maji na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Manispaa ya Songea(Souwasa), kuanza kutekeleza mradi huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa Manispaa hiyo na maeneo mengine ya jirani.
Mjumbe wa Kamati hiyo Pascal Msigwa,amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo,lakini ameiomba Serikali kuharakikisha ujenzi wake ili wananchi waweze kupata huduma ya maji ya uhakika na kuwaondolea adha ya kupata huduma hiyo kwa mgao.
Msimamizi wa mradi huo kutoka Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Songea mjini(SOUWASA) Vicenti Bahemana alisema,mradi ulianza kutekelezwa mwezi Januari 2024 na unatarajia kukamilika mwezi Septemba 2026.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.