Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma Mhe. Ngollo Malenya, ametambua na kuthamini juhudi za wadau mbalimbali wanaopambana kulinda misitu na mazingira ya asili wilayani humo.
Akiwahutubia wananchi na viongozi katika hafla maalum iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kanisa la Romani mjini Namtumbo Mhe. Malenya alitoa pongezi za dhati kwa mashirika na jumuiya zinazotetea uhifadhi, akisema mchango wao unaleta mabadiliko chanya kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Wadau waliotunukiwa heshima hiyo ni pamoja na Honeyguide Foundation, Carbon Tanzania—wanaoendesha miradi ya kaboni—pamoja na jumuiya za misitu ngazi ya kijiji na kata, ambao wamekuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii, kusimamia misitu kwa pamoja, na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala.
Mhe. Malenya alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejikita katika kulinda mazingira na kuhimiza matumizi ya nishati safi kama sehemu ya ajenda ya maendeleo endelevu.
DC Malenya ametoa rai kwa wananchi na wadau wote kuongeza mshikamano katika kuhifadhi rasilimali za taifa, akisema: “Rais Samia ni kinara wa uhifadhi na matumizi ya nishati safi nchini.
Hafla hiyo pia ilitoa fursa kwa wananchi kupata elimu kuhusu miradi ya uhifadhi na manufaa yake kiuchumi, kijamii na kimazingira.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.