Tunawajali, tunajenga mazingira bora ya kusoma – sasa ni zamu yenu kusoma kwa bidii!” – Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma Mhe. Denis Masanja, alitoa kauli hiyo alipofanya ziara rasmi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Masonya na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
Katika hotuba yake yenye hamasa, Mhe. Masanja alieleza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuweka kipaumbele kwenye sekta ya elimu kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya shule kote nchini.
Alibainisha kuwa Shule ya Masonya ni miongoni mwa walionufaika ambapo kwa sasa kuna ujenzi wa bwalo la kisasa la chakula unaoendelea, mradi wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 160 unaotarajiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
“Serikali yenu inawajali, ndiyo maana tunajenga maoweni, madarasa mapya, na sasa bwalo la kisasa. Huu ni ushahidi wa dhamira ya dhati ya Rais Samia kuhakikisha mnafundishwa katika mazingira bora.
Mhe. Masanja aliwatia moyo wanafunzi wa Masonya kujiamini, kuwa na maono makubwa, na kutambua kuwa elimu ni nguzo kuu ya mafanikio
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.