Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile amewataka wananchi kutumia nishati mbadala kwa ajili ya kupikia ili kuondokana na matumizi ya kuni, ambayo husababisha uharibifu wa mazingira na kupoteza uoto wa asili.
Kauli hiyo imetolewa katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Songea (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa HOMSO, Songea. Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali kwa lengo la kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utendaji wa kazi na maagizo ya kikao kilichopita kupitia Halmashauri za Madaba, Songea, na Manispaa ya Songea.
Miongoni mwa mikakati iliyopangwa ili kuleta maendeleo wilayani humo ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi sahihi ya nishati mbadala kama makaa ya mawe, kudhibiti utoro katika shule za msingi na sekondari, na kudhibiti ufugaji holela wa ng’ombe.
Afisa Misitu wa Manispaa ya Songea, Betram Njelekera, amesema kuwa katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita za kudhibiti uharibifu wa mazingira, Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mheshimiwa Damas Ndumbaro amevipa vikundi 12 mitungi ya gesi 84 , ili kusaidia jamii kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.