Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba, wilayani Songea mkoani Ruvuma Ndugu Sajidu Idrisa Mohamed, ametembelea Hospitali ya Halmashauri ya Madaba kwa lengo la kukagua mafanikio ya maboresho makubwa ya huduma za afya yanayoendelea kutekelezwa.
Katika hatua inayoonesha imani kubwa kwa huduma zinazotolewa, Mkurugenzi alijumuika na wananchi kupata matibabu hospitalini hapo.
Akizungumza mara baada ya kutembelea wodi na vitengo mbalimbali, Mkurugenzi Sajidu aliwataka wananchi wa Madaba na watumishi wa umma kutumia kikamilifu huduma bora zinazopatikana hospitalini hapo.
Alisisitiza kuwa huduma nyingi ambazo zamani zililazimu wananchi kusafiri nje ya wilaya, kwa sasa zinapatikana ndani ya hospitali hiyo ya wilaya.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi alitangaza kuwa kuanzia Mei 26 hadi 31, 2025, kutakuwepo na kambi maalum ya madaktari bingwa na mabingwa bobezi, kupitia mpango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kambi hiyo inalenga kuwapatia wananchi huduma za kibingwa kwa urahisi na gharama nafuu.
Wananchi wote wa Madaba na maeneo jirani wametakiwa kufika kwa wingi katika kipindi hicho ili kunufaika na huduma hizo muhimu za kiafya, ambazo zimeletwa karibu na jamii kwa lengo la kuboresha afya na ustawi wa wananchi wa wilaya hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.