Utekelezaji wa jengo la uwekezaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma (Mbinga DC Mall) umeanza kwa lengo la kukuza uchumi wa eneo hilo na kutoa fursa mbalimbali kwa wananchi. Jengo hilo linatarajiwa kuwa kituo kikuu cha biashara, kikihusisha shughuli nyingi zenye tija kwa jamii na kuongeza mapato ya halmashauri.
Mbinga DC Mall litajumuisha huduma na biashara mbalimbali kama maduka ya bidhaa, saluni za kisasa, maeneo ya burudani kama bar, pamoja na michezo ya watoto. Uwepo wa jengo hili utasaidia kuongeza ajira, kuvutia wawekezaji na kuboresha mandhari ya mji wa Mbinga kuwa wa kisasa zaidi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.