• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MBOLEA ya ruzuku yaipandisha kahawa nyasa kwa kiwango cha juu

Imewekwa kuanzia tarehe: June 7th, 2025

Wakulima wa zao la kahawa katika kijiji cha Mpepo, Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wamefurahia mafanikio makubwa yaliyotokana na msaada wa mbolea ya ruzuku inayotolewa na Serikali. Mbolea hiyo imeleta mapinduzi makubwa kwenye kilimo cha kahawa kwa kuongeza uzalishaji na kupunguza gharama za uzalishaji, huku pia ikiongeza ajira kwa vijana na wanawake kupitia kuongezeka kwa mahitaji ya nguvu kazi mashambani.

Ilbert Mahai, mkulima mwenye shamba la ekari 19 katika kijiji cha Mpepo, amesema amepata mafanikio makubwa baada ya kuanza kutumia mbolea ya ruzuku. Ameongeza uzalishaji kutoka tani 20 msimu wa 2022/2023 hadi zaidi ya tani 150 msimu wa 2024/2025. Mahai anatarajia kuvuna tani 200 katika msimu ujao kutokana na maandalizi ya mapema yaliyowezeshwa na upatikanaji wa mbegu na pembejeo kupitia Chama cha Ushirika Mapendo.

Kwa upande wake, Alto Matembo kutoka kijiji cha Ndondo amesema zao la kahawa limemwezesha kujenga nyumba bora na kuwasomesha watoto hadi chuo kikuu. Amewashauri vijana wa Nyasa wajikite kwenye kilimo cha kahawa ambacho kwa sasa kina tija kubwa baada ya bei kupanda kutoka Sh.4,500 hadi Sh.10,000 kwa kilo moja. Aidha, ameihimiza Serikali kuendelea kutoa pembejeo kwa wakati na kudhibiti gharama za usafirishaji wa pembejeo hizo.

Mkulima Method Ngonyani kutoka Mtetema ameipongeza Serikali kwa kuanzisha mradi wa miche bora ya kahawa ya aina ya Kombat, ambayo inasambazwa bure kupitia Halmashauri na Bodi ya Kahawa Tanzania. Mradi huo umewasaidia wakulima wengi kuachana na mazao yasiyo na faida kama mahindi na maharage, na kuelekeza nguvu zao kwenye kahawa yenye tija zaidi.

Katibu wa Chama cha Msingi cha Ushirika Mapendo, Panglas Komba amesema wamefanikiwa kununua mtambo wa kuchakata kahawa unaohudumia wakulima 200 kwa wakati mmoja. Hata hivyo, amesema changamoto ni uwezo mdogo wa mtambo huo ukilinganisha na mahitaji makubwa ya wakulima. Ameiomba Serikali kuwasaidia mashine yenye uwezo mkubwa zaidi ili kuongeza ubora na wingi wa kahawa itakayowahi soko la minada kwa bei nzuri.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBOLEA ya ruzuku yaipandisha kahawa nyasa kwa kiwango cha juu

    June 07, 2025
  • NMB yawasha moto Peramiho;Bonanza lenye elimu ya fedha na michezo lavutia wengi

    June 07, 2025
  • MBINGA DC Mail kuleta mapinduzi ya Biashara na ajira wilayani Mbinga

    June 07, 2025
  • MAPUMZIKO mema ya Sikukuu

    June 07, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.