• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MICHE ya kisasa ya kahawa 23,275 itakavyoimarisha mapato na kuboresha ushirika wa MBIFACU

Imewekwa kuanzia tarehe: July 8th, 2020

CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Wilaya za Mbinga na Nyasa (MBIFACU) katika msimu wa mwaka 2020/2021  kinatarajia kuongeza hekari 20 za miche ya kahawa ya kisasa(Compact) na kufikisha jumla ya hekari 71 za kahawa katika shamba la Ugano Mbinga .                                                          

Kaimu Meneja wa  wa MBIFACU Henrick Ndimbo amesema upanuzi wa shamba la kahawa Ugano umelenga kuimarisha vitega uchumi wa MBIFACU na kuongeza mapato ya chama hicho ili kuweze kujitegemea na kuimarisha ushirika.

Ndimbo amesema  miche ya kisasa ya kahawa katika hekari hizo 20 ipo 23,275  imepandwa msimu huu na kwamba mwaka 2023 MBIFACU inatarajia kuzalisha kahawa tani zaidi ya 23,000 ambazo zitawaingizia sh.milioni 69 ambazo zitaongeza mapato ya ndani ya chama.

Naye Kaimu Makamu Mwenyekiti wa MBIFACU Winfred Lupembe amesema shamba hilo la kisasa la kahawa litaimairisha uchumi wa chama hicho na hatimaye MBIFACU itajitegemea kwa kila kitu kutokana na rasilimali zake.

Amesema katika shamba jipya miche ya kahawa imefunikwa kwa majani ili kuilinda miche hiyo wakati wa baridi na wakati wa jua kali isipate mwanga mkali na kuathiri miche kuwa na rangi ya njano ambayo inapoteza ubora wa kahawa.

‘’Shughuli zote ambazo tunazifanya MBIFACU zinalenga kuongeza ajira kwa vijana katika Wilaya ya Mbinga,lakini jambo kubwa zaidi ni  kuunga mkono juhudi za  Rais John Magufuli kwa kauli yake ya kuimarisha ushirika nchini’’,alisisitiza Lupembe.

Akizungumzia historia  ya shamba hilo Kaimu Meneja wa MBIFACU Henerick Ndimbo anasema katika kijiji cha Ugano, wanamiliki eneo la hekari 1052 na kwamba bado wana shamba la zamani la kahawa lenye ukubwa wa hekari 50  ambalo lina miche ya kahawa yenye umri wa zaidi ya miaka 100,

Hata hivyo amesema walipokabidhiwa miche hiyo kutoka Chama Kikuu cha Ushirika cha MBICU,waliamua kuifufua upya miche hiyo na kuacha baadhi ya miche ya zamani  inayotumika kama shamba darasa.

“Hii miche ya zamani ya kahawa ukiitunza vizuri inaweza kutoa hadi kilo tano kwa mche mmoja,msimu uliopita tuliweza kupata hadi tani 2.6 za kahawa kwa miche ya zamani ambazo zilituingizia milioni tisa.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa MBIFACU Winfred Lupembe amesema katika kuliboresha shamba la zamani la kahawa  chama hicho kina mpango wa kufuga ng’ombe ambao watawawezesha kupata mbolea ya samadi ambayo itatumika kuweka kwenye kahawa.

Lupembe amesisitiza kuwa  shamba hilo baada ya muda sio mrefu litabadilika na kustawi hali ambayo itaongeza uzalishaji wa kahawa na kwamba MBIFACU katika shamba hilo pia inatarajia kupanda migomba ambayo itakuwa zao la biashara  katika kuongeza mapato kwa Chama hicho.

Mrajisi Msaidizi wa  Vyama vya Ushirika Mkoani Ruvuma Bumi Masuba anatoa rai kwa Vyama vya ushirika nchini kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ili viwe na vyanzo vingine vya mapato badala ya kutegemea ushuru wa mazao ya mkulima.

“Msimu  uliopita Chama Kikuu cha Ushirika MBIFACU kilikuwa kinatoza ushuru shilingi 40 kwa kilo,kutokana na uboreshaji wa miradi ya chama,ushuru umeshushwa kuanzia Julai mosi 2020,mkulima anatozwa sh. 30 kwa kilo na tutaendelea kushusha kadri miradi ya uwekezaji itakavyoimarika’’,alisisitiza.

Amesema miradi kwa vyama vya ushirika pia ina muongezea mkulima mapato kwa  kuwa na gawio la faida kwa sababu kadiri  vyama vinavyoongeza mapato ndiyo inavyotengenezwa faida kwa mkulima.

 MBIFACU inamiliki shamba lenye ukubwa wa hekari 1052 katika eneo la Ugano,ambapo baadhi ya maeneo wameweka  wawekezaji wanaoendeleza likiwemo shamba la kahawa ya TACRI Ugano.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Julai 8,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBOLEA ya ruzuku yaipandisha kahawa nyasa kwa kiwango cha juu

    June 07, 2025
  • NMB yawasha moto Peramiho;Bonanza lenye elimu ya fedha na michezo lavutia wengi

    June 07, 2025
  • MBINGA DC Mail kuleta mapinduzi ya Biashara na ajira wilayani Mbinga

    June 07, 2025
  • MAPUMZIKO mema ya Sikukuu

    June 07, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.