Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma umetambulisha mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 962.7.
Mradi huu unalenga kutatua changamoto ya maji safi na salama katika vijiji vya Mbanga na Kigongo, kata ya Lumeme.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Peres Magiri, amemtaka mkandarasi kuhakikisha mradi unajengwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati. Amesisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata maji safi, hivyo fedha zilizotengwa ziendane na thamani halisi ya mradi.
Mradi huu unatarajiwa kuhudumia wananchi 4,990 kutoka vijiji vya Mbanga na Kigongo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.