Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akiambatana na Katibu wa Tume ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Bw. Kailima Ramadhani leo Januari 03, 2025 wamemtembelea ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ambapo pamoja na mambo mengine walimpa taarifa ya uwepo wa zoezi la uboreshaji wa daftari la Kudumu la Mpiga Kura Januari 12 hadi 18, 2025 katika mkoa wa Ruvuma kwenye Halmashauri za Nyasa, Mbinga, Mbinga Mjini, Songea na Songea Mjini.
Pia ujumbe huo uliambatana na baadhi ya wajumbe wa Managementi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.