• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

NMB yaleta mapinduzi ya elimu ya kifedha Peramiho,yawakutanisha wanavikundi zaidi ya 50 kwa mafunzo na michezo

Imewekwa kuanzia tarehe: June 7th, 2025

Katika hatua ya kuhamasisha uelewa wa masuala ya kifedha kwa wananchi wa vijijini, Benki ya NMB imeendesha mafunzo kabambe ya elimu ya kifedha kwa zaidi ya vikundi 50 katika kata ya Peramiho, Halmashauri ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma.

 Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo viongozi wa vikundi vya kijamii ili waweze kusimamia vizuri fedha, kuweka akiba na kutumia huduma za kibenki kwa tija.

Tukio hilo lililovuta mamia ya wananchi wa Peramiho, lilichangamka zaidi kwa michezo ya ukakamavu iliyoambatana na mafunzo hayo ikiwemo kuvuta kamba, mbio za magunia, netiboli na mpira wa miguu.

Michezo hiyo ililenga kuimarisha mshikamano wa kijamii, kuhamasisha ushiriki wa vikundi na kutoa ujumbe wa mshikamano katika maendeleo ya kiuchumi.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo,Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Kusini, Roman Degeleki, alieleza kuwa benki hiyo imejipambanua kwa kuwafikia Watanzania wote hadi ngazi za vijiji.

 “NMB ni benki inayowafuata wateja popote walipo. Tuna mawakala zaidi ya 7,000 nchini ambao wanahakikisha huduma zetu zinapatikana hata sehemu zisizofikika kirahisi,” alisema kwa msisitizo.

Naye Afisa Mahusiano wa NMB Tawi la Masasi, Fanueli Duya, alitoa shukrani kwa wateja wa benki hiyo na kuwataka kutumia fursa ya kufungua akaunti mpya kupitia kampeni yao endelevu ya “Fungua Akaunti, Jenga Maisha Yako.”

Alibainisha kuwa huduma hiyo inalenga kuongeza ujumuishwaji wa wananchi katika mfumo rasmi wa kifedha.

Hatua ya NMB kutoa mafunzo haya inathibitisha dhamira ya kweli ya benki hiyo katika kuinua maisha ya wananchi kwa vitendo.

Kwa kuwajengea uwezo viongozi wa vikundi mashinani, NMB inachochea maendeleo ya kiuchumi, inaimarisha elimu ya kifedha na kuleta mapinduzi ya kibenki vijijini.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBOLEA ya ruzuku yaipandisha kahawa nyasa kwa kiwango cha juu

    June 07, 2025
  • NMB yawasha moto Peramiho;Bonanza lenye elimu ya fedha na michezo lavutia wengi

    June 07, 2025
  • MBINGA DC Mail kuleta mapinduzi ya Biashara na ajira wilayani Mbinga

    June 07, 2025
  • MAPUMZIKO mema ya Sikukuu

    June 07, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.