Katika taswira isiyo ya kawaida lakini yenye ujumbe mzito wa upendo na matumaini, wananchi wa eneo la Pacha ya Likuyu Kata ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameamua kuonesha hisia zao kwa njia ya kipekee.
Juu ya mti mkubwa uliopo katikati ya eneo hilo, wamelipamba tawi lake kuu kwa picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ishara ya shukrani ya dhati kwa maendeleo yanayoendelea kushuhudiwa wilayani humo.
Kwa wakazi wa eneo hili, mti huo haukuwa wa kawaida tena umegeuka kuwa “mnara wa matumaini”, wakiitazama picha hiyo juu ya mti kama alama ya mapinduzi ya kijamii na kiuchumi yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita.
Wananchi hao wamesema wameweka picha hiyo si kwa heshima tu, bali kama sauti isiyo na maneno inayoonesha jinsi walivyoguswa na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika kwenye sekta za afya, elimu, barabara na maji sekta ambazo zamani zilikuwa changamoto kubwa kwao.
“Tumeamua kuiweka picha ya Mama yetu Rais Samia juu ya mti huu mkubwa kwa sababu yeye ni taa yetu ya maendeleo,” alisema mmoja wa waendesha bodaboda kwa hisia.
“Hatukuwa na barabara, sasa tunayo. Hatukuwa na maji, sasa bomba linapita. Hili ni jambo la kumshukuru.” Kauli hii imejikita mioyoni mwa wananchi wengi ambao sasa wanaishi maisha yaliyojaa matumaini mapya kutokana na uboreshwaji wa huduma za msingi.
Kwao, Rais Samia si kiongozi tu bali ni chombo cha mabadiliko na dira ya maisha bora. Imani yao ni kuwa mwamko huu wa maendeleo hautaishia Namtumbo tu, bali utazidi kufungua fursa nyingi zaidi kwa mikoa yote ya pembezoni.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.