Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa fedha kwaajili ya kukarabati hospitali kongwe ya wilaya ya Tunduru iliyojengwa mwaka 1930.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Dr. Bernad Mwamanda, ameeleza kuwa wamefanikiwa kujenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ambalo limegharimu milioni 900, na jengo la wagonjwa wa dharura (EMD) ambalo mwanzo halikuwepo limegharimu milioni 300.
Ameongeza kuwa majengo hayo yamekamilika, yanaendelea kutoa huduma na yana vifaa tiba ambavyo vinasaidia sana kwenye matukio ya dharura, pia wamepatiwa gari la kubebea wagonjwa ambapo awali walilazimika kuazima kutoka kituo kingine.
Mkazi wa Wilaya ya Tunduru, Sara Chifu, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuboresha majengo ya hospitali na sasa ubora wa huduma zote ni mzuri na zinapatikana kwa wakati.
Kwa upande wake, mkazi mwingine wa wilaya hiyo, Juma Mahamba, amesema kuwa ukilinganisha awali na sasa, uboreshaji wa sasa umekuwa bora zaidi tofauti na awali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.