• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TAKUKURU Ruvuma yakagua miradi ya bilioni 5.4

Imewekwa kuanzia tarehe: April 28th, 2022

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imekagua miradi mbalimbali ya Zaidi ya shilingi bilioni tano katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi 2022.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa miezi mitatu ya Taasisi hiyo kwa wanahabari mjini Songea,Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Janeth Haule,amesema TAKUKURU imefuatilia miradi hiyo ikiwemo fedha za utekelezaji  miradi ya maendeleo kupitia UVIKO 19.

Ameitaja miradi iliyofuatiliwa kuwa ni ujenzi wa vyumba nane vya madarasa katika shule za sekondari Ruhuwiko,Mbambi,Ruanda na Mbinga Girls zilizopo katika wilaya ya Mbinga.

“TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha Januari hadi Machi 2022,imeweza kutekeleza majukumu yake ya uchunguzi na kufanikiwa kupokea jumla ya taarifa mpya 45 za malalamiko mbalimbali,kati ya hayo,malalamiko 33 yalikuwa na viashiria vya rushwa na yote yalifanyiwa uchunguzi wa awali’’,alisisitiza Haule.

Hata hivyo amesema kwa upande wa mashtaka katika kipindi cha miezi mitatu,TAKUKURU Ruvuma imeweza kufungua kesi moja ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Wilaya ya Mbinga inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na kufanya jumla ya kesi sita kuendeshwa mahakamani.

Kwa upande wa uzuiaji Rushwa,Naibu Mkuu wa TAKUKURU huyo amesema Taasisi yake imefanikiwa kufanya uchambuzi wa mifumo sita kuhusu utendaji kazi wa Wakala wa Manunuzi ya Serikali (GPSA) na Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA).

Hata hivyo amesema viashiria vya rushwa ya ngono  katika sekta ya elimu vimejitokeza katika Halmashauri za Manispaa ya Songea,Halmashauri za Wilaya ya Songea,Tunduru na Namtumbo.

Matarajio ya TAKUKURU Ruvuma katika kipindi cha miezi mitatu ijayo ameyataja kuwa ni pamoja na kuendelea kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua wale wote watakaokutwa na tuhuma za vitendo vya rushwa na kuwafikisha mahakamani.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari,Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Aprili 28,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBOLEA ya ruzuku yaipandisha kahawa nyasa kwa kiwango cha juu

    June 07, 2025
  • NMB yawasha moto Peramiho;Bonanza lenye elimu ya fedha na michezo lavutia wengi

    June 07, 2025
  • MBINGA DC Mail kuleta mapinduzi ya Biashara na ajira wilayani Mbinga

    June 07, 2025
  • MAPUMZIKO mema ya Sikukuu

    June 07, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.