Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amesema mkoa wa Ruvuma una vivutio vingi vya uwekezaji ambavyo vinaweza kuwa vyanzo vikubwa vya mapato zikiwemo sekta za madini, kilimo na biashara.
Amesema hayo wakati akifungua kikao cha Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi na Wafanyabiasha na Wadau Mbalimbali wa Kodi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
"Tuna sekta ya madini, kilimo, biashara, uvuvi, mifugo, tunao wakulima, wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa na vyanzo vingine mbalimbali ambavyo vinachangia pato la taifa, pia maendeleo ya mkoa wetu,"alisema Kanali Ahmed.
Ameongeza kuwa Kodi sio jambo linalompendeza kila mtu lakini endapo wananchi watatengenezewa mazingira mazuri na kuitambua vizuri wanaweza kuwa wadau wazuri wa kulipa Kodi.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Maboresho ya Kodi nchini, Balozi Maimuna Tarishi, amesema tume hiyo iliundwa kufuatia malalamiko ya muda mrefu ya wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji kutokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo ambazo zinahusisha mfumo wa kodi nchini ikiwemo wingi wa kodi, uwepo wa mamlaka nyingi za ukussanyaji kodi pamoja na ukadiria wa kodi.
Amesema tume hiyo inapokea maoni na mapendekezo kutoka kwa walipaji kodi kote nchini ambayo yatawasaidia kuchakata taarifa zote zilizokusanywa ili kupata mfumo bora na ambao wamekubaliana kwa pamoja kwa sababu itakuwa ni sehemu ya maoni yao.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, mapendekezo yanayotolewa yanalenga sheria zinazohitaji kufanyiwa maboresho, mapungufu ya usimamizi wa ukusanyaji kodi, changamoto za urasimishaji biashara hivyo mwananchi ili aweze kulipa kodi ni lazima awe na mazingira rafiki ya kufanya biashara na kuwezeshwa katika uzalishaji.
Wananchi wanaweza kutoa maoni yao kuhusu maboresho ya kodi ambayo yatapokelewa na Tume hiyo kupitia Dodoso: https://edodoso.gov.go.tz/544978, Simu (Whatsapp na SMS): 0748 755 677, 0738 588 813, 0682 288 784 pamoja na Baruapepe: maboresho.kodi@gmail.com.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.