• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UCHANGIAJI damu wazidi kuimarika Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: June 4th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amesema katika mkoa wa Ruvuma takwimu za ukusanyaji wa damu zimeonyesha kuwa na mafanikio na kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha maandalizi kuelekea kilele cha wiki ya uchangiaji wa hiari wa Damu Salama ambacho hufanyika Juni 14 kila mwaka, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.

"Mwaka 2022 chupa za damu zilikusanywa 3,600 sawa na asilimia 24.5 ya mahitaji, zilifanyiwa vipimo maabara na kusambazwa, idadi hii imeongezeka hadi kufikia chupa 12,278 sawa na asilimia 83 ya mahitaji kwa mwaka 2023, kufikia chupa 7,016 sawa na asilimia 47.4 ya mahitaji ya mkoa kwa mwaka 2024, katika kipindi cha Januari hadi Mei 2025 Mkoa umekusanya chupa 2,952 sawa na asilimia 20 ya lengo la mwaka yaani chupa 14,789 bado haujakidhi mahitaji," alisema Makondo.

Ameeleza kuwa ili kukabiliana na hali hiyo Serikali imeimarisha upatikanaji wa huduma za damu salama kwa kununua majokofu, amesema mkoa una vituo 37 ambavyo vinatoa huduma ya Damu Salama, vituo 26 sawa na asilimia 70 vinamilikiwa na Serikali wakati vituo 11 sawa na asilimia 30 vinamilikiwa na taasisi za dini (FBO).

Makondo amebainisha kuwa watumiaji wakubwa wa damu ni watoto walio chini ya miaka mitano ambao wanatumia damu inayokusanywa kwa asilimia 50, mama wajawazito ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua wanatumia asilimia 30 ya damu inayokusanywa, lakini wahanga wa ajali, wagonjwa wa magonjwa ya ndani na wanaopata tiba kwa njia ya upasuaji ambao wakati mwingine hupoteza damu wote kwa pamoja wanatumia asilimia 20 ya damu inayokusanywa.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dr. Louis Chomboko, amesema bado kuna uhitaji mkubwa wa damu kutokana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika jamii zikiwepo ajali za barabarani.

Ametoa wito kwa wananchi katika Halmashauri zote za mkoa wa Ruvuma kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wahitaji wa damu salama, akisisitiza zoezi hilo kwa mwaka huu 2025  tayari limeanza Juni 1 na linatarajiwa kumalizika Juni 14.

Wiki ya Uchangiaji wa Hiari wa Damu Salama hufanyika kila mwaka duniani kote kuanzia Juni 1 hadi 14, ikiwa na lengo la kuhamasisha uchangiaji wa damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wenye uhitaji. Kauli mbiu ya mwaka huu inasema: 'Changia Damu, Leta Matumaini; Pamoja Tunaokoa Maisha.'

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBOLEA ya ruzuku yaipandisha kahawa nyasa kwa kiwango cha juu

    June 07, 2025
  • NMB yawasha moto Peramiho;Bonanza lenye elimu ya fedha na michezo lavutia wengi

    June 07, 2025
  • MBINGA DC Mail kuleta mapinduzi ya Biashara na ajira wilayani Mbinga

    June 07, 2025
  • MAPUMZIKO mema ya Sikukuu

    June 07, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.