Maafisa wa Dawati la Huduma za Msaada wa Kisheria Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma wameratibu mafunzo ya kujengeana uwezo na uelewa wa kisheria kwa viongozi wa Serikali wa Kata ya Bethrehem.
Mafunzo hayo yameangazia Sheria ya Mirathi, Uandishi wa Wosia, Matunzo ya Watoto, pamoja na Ukatili wa Kijinsia, sambamba na mbinu za kuepuka na kukabiliana na changamoto hizo.
Washiriki wa mafunzo hayo ni wenyeviti wa mitaa, wajumbe wa serikali za mitaa, mabalozi, Mhe. Diwani, viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya kata, pamoja na watendaji wa mitaa.
Wadau mbalimbali pia wamehudhuria, wakiwemo maafisa wa Dawati la Jinsia na Watoto la Polisi Mbinga pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.