7.1 WAKALA WA HIFADHI YA CHAKULA KANDA YA SONGEA (NFRA)
Taarifa ya utekelezaji wa kazi za wakala wa hifadhi ya chakula – NFRA kuanzia Julai 1, 2022 hadi 30 Novemba 2022
i. Ununuzi Msimu wa 2022/2023
Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kupitia kanda ya Songea ilipangiwa kununua jumla ya tani 25,000 za mahindi. Kutokana na upatikanaji mdogo wa nafaka kwa msimu huu wa 2022/2023 kanda ilipewa idhini ya kununua tani 6000 kwa kuanzia. Aidha, kuanzia tarehe 21 Septemba, 2022 kanda ilipewa idhini ya kununua tani 3000 za nyongeza ili kuendelea na zoezi la kuongeza akiba ya chakula kwa ajili ya kukabiliana na majanga mbalimbali.
ii. Njia za Ununuzi Zilizopagwa
Kutokana na ushindani katika soko kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Wakala ulipanga kutumia njia kuu tatu za ununuzi ambazo ni:-
i) Kununua kwa njia ya vituo vya ununuzi
ii) Kununua kwa njia ya vikundi vya wakulima vya ushirika.
iii) Kununua kwa kutumia mawakala.
iii. Mpango wa Ununuzi
Wakala ulipanga kiwango cha ununuzi kwa Halmashauri saba zilizopo Mkoa wa Ruvuma kwa kuzingatia uwiano wa taarifa za matarajio ya uzalishaji wa ziada ya mahindi. Aidha, kutokana na upatikanaji mdogo wa nafaka kwa mwaka huu, mgawanyo huo haukufuatwa.
iv. UNUNUZI
Kanda ya Songea ilianza ununuzi katika maeneo yote ya Mkoa wa Ruvuma kuanzia tarehe 05/08/2022 na mpaka kufikia tarehe 30/11/2022, kanda ilikuwa imenunua tani 7,098.283 zenye thamani ya shilingi 5,168,367,960/= kutoka katika vituo vya ununuzi vya kudumu 11 na vile vya muda 5 pia ununuzi ulifanyika kupitia mawakala 6 na kuleta jumla ya vituo 22.
V. Bei za Ununuzi
Mahindi yalinunuliwa kwa bei kati ya shilingi 650 na 780. Mabadiliko ya bei za kununulia zilibadilika mara kwa mara kutokana na ushindani wa bei zilizokuwa sokoni. Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ulifanya mabadiliko ya bei ili kuongeza akiba ya Taifa ya chakula kwa lengo la kuihakikikishia Nchi inakuwa na uhakika wa chakula kukabiliana na majanga mbalimbali hasa ukame uliojitokeza katika baadhi ya maeneo ya nchi.
vi. Mafanikio
a) Hadi kufikia tarehe 30 Novemba 2022, NFRA ilikuwa imefanikiwa kununua tani 7098.283 za mahindi sawa na asilimia 28.4 ya tani 25,000 zilizopangwa kununuliwa katika msimu wa 2022/2023.
b) Serikali kupitia NFRA iii nufaisha wakulima kwa kuongeza bei ya kununulia mahindi kadri wafanyabiashara walivyoongeza bei sokoni hadi kufikia kikomo cha bei ya shilingi 780 kwa kila kilo hivyo kuwasaidia wakulima kujiingizia kipato cha kununulia p na kurudi shambani.]
c) Kutengeneza ajira kwa vijana takribani 450 waliotumika kwenye zoezi la ununuzi
d) Kusaidia serikali kukusanya kodi ya zuio yenye jumla ya shilingi 103,367,359.20 ambapo hadi Novemba 30 2022 kiasi cha shilingi 69,997,898 kilikuwa kimelipwa kwa kamishina wa TRA. Aidha jumla ya shilingi 155,051,038.80 Kitalipwa kwa Halmashauri kama ushuru wa mazao (crop ces).
vii. Changamoto
Ufinyu wa nafaka ya mahindi sokoni kwa msimu huu wa 2022/2023 kulikosababishwa na mahitaji ya nafaka ya mahindi kuwa kubwa sana.
NFRA kutumia muda mrefu kununua tani 7098.283 tu ukilinganisha na misimu mingine hivyo, kuongeza gharama za uendeshaji
Baadhi ya wakulima/ wafanyabiashara kuleta vituoni nafaka ambazo hazikizi viwango vya ubora.
viii. Hitimisho
Mwisho, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula unaishukuru Serikali kwa ujumla kuwezesha kutekeleza jukumu la ununuzi wa mahindi kwa kutenga fedha za kutosha kununua mahindi ya wakulima kwa njia mbalimbali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.