WATU 1,257,180 sawa na asilimia 70 ya wakazi wote wa Mkoa wa Ruvuma hadi kufikia Novemba 2022 wanapata huduma ya maji safi na salama.
Kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022,Mkoa wa Ruvuma una jumla ya watu 1,848,794.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amelitaja lengo la Mkoa ni kuhakikisha wanatoa huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 85 kwa wakazi waishio vijijini na asilimia 95 kwa wakazi waishio mjini ifikapo mwaka 2025.
Akizungumzia huduma ya maji mijini,Kanali Thomas amesema Mkoa wa Ruvuma una miji sita ambayo ni makao makuu ya Halmashauri za Songea,Mbinga,Madaba,Tunduru,Namtumbo na Mbambabay.
Hata hivyo amesema hadi kufikia Oktoba 2022,huduma ya maji safi na salama katika makao makuu ya miji hiyo ilikuwa ni asilimia 72.7.
Ameitaja idadi ya watu wanaopata huduma ya maji safi na salama vijijini mkoani Ruvuma kuwa ni asilimia 68 sawa na watu 1,005,745 kulingana na sensa ya watu yam waka 2022.
“Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mkoa wa Ruvuma ulitengewa zaidi ya shilingi bilioni 16 kwa ajili ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maji’’,alisisitiza Kanali Thomas.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga amesema vijiji 525 kati ya vijiji 551 vinavyohudumiwa na RUWASA mkoani Ruvuma, vinapata huduma ya maji safi na salama na kwamba hadi sasa ni vijiji 170 mkoani Ruvuma havina huduma ya maji.
Hata hivyo amesema hadi kufikia Novemba 30,2022,Mkoa wa Ruvuma ulikuwa unatekeleza miradi ya maji 32 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 51 na kwamba miradi hiyo itakapokamilika itahudumia zaidi ya wakazi 264,000 wa vijiji 81.
Huduma ya maji safi na salama katika Mkoa wa Ruvuma inatolewa na Jumuiya za watoa huduma ya maji ngazi ya jamii ambapo hadi sasa Mkoa una jumuiya 116
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.