• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BILIONI 230 zinavyoteleza miradi ya TANROADS Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: June 14th, 2023

SERIKALI imetoa zaidi ya shilingi bilioni 230 kutekeleza miradi mbalimbali ya kitaifa ya Barabara na madaraja mkoani Ruvuma

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma,Mhandisi Ephatar Mlavi amesema kati ya fedha hizo zaidi ya shilingi bilioni 129 zimetumika kujenga Barabara ya lami nzito yenye urefu wa kilometa 66 kutoka Mbinga hadi Mbambabay wilayani Nyasa.

Amesema mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2018  kupitia kampuni ya China Henan International Cooperative Group ltd na ulikamilika mwaka 2021 hivyo kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji mkoani Ruvuma.

Ameutaja mradi mwingine ambao umekamilika kwa asilimia 100 kuwa ni wa ujenzi wa daraja la Mto Ruhuhu unaomwaga maji yake katika ziwa Nyasa ambapo serikali ilitoa shilingi bilioni 8.9 kujenga daraja hilo mradi ambao unaunganisha wilaya za Nyasa mkoani Ruvuma na wilaya ya Ludewa wilayani Njombe.

Mhandisi huyo wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma ameutaja mradi mwingine wa kitaifa kuwa ni ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Songea ambao upo Ruhuwiko ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 37 kutekeleza mradi huo ambao unatumika na kutoa huduma zote.

Hata hivyo amesema serikali ya Awamu ya Sita pia inatekeleza mradi wa ujenzi wa Barabara ya lami nzito kutoka Kitai hadi Lituhi ambapo kwa kuanzia mradi unatekelezwa kutoka Amanimakoro hadi Ruanda yenye urefu wa kilometa 35.

Amesema mradi unatekelezwa na na Mkandarasi Kampuni ya China Railway Seventh Group ambayo ilianza kutekelezwa Juni 2022 na unatarajiwa kukamilika Desemba 2023 kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 60.

Hata hivyo amesema mradi wa Barabara Kitai hadi Lituhi sehemu ya Ruanda hadi Ndumbi yenye urefu wa kilometa 50 utahusisha ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami na kwamba zabuni imeshatangazwa na mradi  unatarajia kuanza  wakati wowote.

Akizungumzia mradi wa kitaifa wa ujenzi wa Barabara ya lami nzito kutoka Likuyufusi hadi Mkenda yenye urefu wa kilometa 60,Mlavi amesema mzabuni ameshatangazwa na serikali imetoa shilingi bilioni  60 kuanza kutekeleza mradi huo.

Mradi mwingine wa kitaifa unaosimamiwa na TANROADS ameutaja kuwa ni ujenzi wa Barabara ya Songea hadi Makambako kwa kiwango cha lami nzito sehemu ya Songea hadi Lutukira ikijumuisha sehemu ya Mtwara Korido mjini Songea yenye urefu wa kilometa 111.

Mhandisi Mlavi amesema serikali tayari imeshaingia makubaliano na mfadhili Benki ya Dunia kuanza kutekeleza mradi huo na kwamba hivi sasa mradi upo katika hatua za awali za manunuzi.

Kulingana na Meneja huyo wa TANROADS mradi mwingine wa kitaifa unaosimamiwa na TANROADS ni ujenzi wa Barabara ya Lumecha,Londo hadi Kidatu mkoani Morogoro yenye urefu wa kilometa 512 ambao ukikamilika utaunganisha Mkoa wa Ruvuma na Morogoro.

Amesema mradi huo upo katika hatua ya kupitia zabuni za wakandarasi na kwamba mradi utatekelezwa kwa kutumia mtindo wa usanifu ambapo utekelezaji wake unatarajia kuanza wakati wowote baada ya hatua za manunuzi kukamilika.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  wa Ruvuma

Juni 13,2023

                                         

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.