Serikali kupitia wizara ya kilimo imetenga shilingi bilioni 43 katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 kwaajili ya uzalishaji wa mbegu katika sekta ya kilimo nchini
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Kilimo, Mheshimiwa Antony Mavunde, kwenye mkutano wa wadau wa tasnia korosho uliofanyika kwenye ukumbi wa bombambili songea,kuwa lengo serikali kuacha kuagiza mbegu nje ya nchi ili kuikuza sekta ya kilimo nchini
Alisema bajeti hiyo imeelekezwa kwa wakala wa uzalishaji mbegu nchini, ambapo bajeti imeongezeka toka bilioni 10.5 kwa mwaka wa fedha uliopita hadi kufikia bilioni 43 lengo ni kuhakikisha mashamba yote makubwa yaliopo chini ya ASA yanazalisha mbegu kwa wakati
“Tumeamua safari hii yakwamba tutaweka miundo mbinu kwenye mashamba yetu yote makubwa ninavyozungumaza hivi sasa tumeshafungua zabuni katika mashamba ya TARI ya utafiti wa mbegu na zabuni imeshafunguliwa Septemba 5 mwaka huu na mdaa sio mrefu kazi hiyo itaanza” alisema Mavunde.
Hata hivyo Mavunde amesisitiza kuwa moja ya kipimo ni uwezo wa nchi kujitegemea katika uzalishaji wa mbegu bora na wizara imeanza mkakati huo na anaamini kama wizara itafikia malengo .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.