Uzinduzi wa Bonanza la NMB wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma limeibua wanachama wapya wa Klabu za Simba na Yanga.
Akizungumza kwenye Bonanza hilo lililofanyika kwenye kiwanja cha Michezo cha CCM ,Meneja wa NMB Tawi la Namtumbo Julietha Ndazi amesema kupitia NMB,Bonanza hilo limewezesha kusajiri wanachama 70 wa Yanga na kufungua akaunti 80 za mashabiki wa Simba.
Ametoa rai kwa mashabiki wa Yanga na Simba kuendelea kujiunga kuwa wanachama kupitia NMB na kufungua akaunti za timu zao .
Hata hivyo amesema mwamko wa kufungua mashina ya timu hizo ni mkubwa katika wilaya ya Namtumbo ambapo amesema NMB ipo tayari kuwafuata popote walipo ili kuwasajiri na kufungua akaunti za timu zao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.