Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komred Oddo Mwisho amewataka watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuongeza kasi ya kuwaunganishia umeme wananchi wa Wilaya ya Mbinga ambao wanahitaji huduma hiyo muhimu ambayo inachochea maendeleo.
Mwisho ametoa agizo hilo wakati anazungumza na wataalam mbalimbali wa wilaya hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga kwenye kikao maalum kilichofanyika mjini Mbinga.
“Mmefanya kazi nzuri ya kusambaza umeme maeneo mengi ya Wilaya ya Mbinga lakini kuna maeneo ambayo bado hamjayafikia hivyo mnapaswa kuongeza kasi,” alisema Komred Mwisho.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.