Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma imefanya ziara ya siku mbili, kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea katika halmashauri hiyo. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Shule za Msingi za Magwamila, Jenista, Mbiro, na Ulamboni, pamoja na Shule ya Sekondari ya Magagura.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Simon Kapinga, alilitaja lengo kuu ni kufuatilia maendeleo ya miradi hiyo, kuhakikisha utendaji bora, na kuweka nguvu mahali panapohitaji marekebisho.
Amehimiza umuhimu wa kasi ya utekelezaji wa miradi, hasa katika kipindi hiki cha mvua, ili kufanikisha malengo kwa wakati.
“Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kukamilisha miradi hii, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunakamilisha kwa wakati na kwa viwango vya ubora vinavyohitajika,” alisema Mhe. Kapinga.
Ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kutatua changamoto za wananchi na kuweka kipaumbele katika maendeleo ya jamii.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.