KAMATI za Usalama (KU) kutoka Wilaya zote Mkoani Ruvuma zimepongezwa kwa kufanikisha ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Ruvuma iliyofanyika katika wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma kuanzia Septemba 23 hadi 29 mwaka huu.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed wakati anazungumza na Kamati hizo mjini Songea ambapo amesema Kamati hizo zimefanikisha ziara ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kufanyika kwa amani,usalama utulivu.
Hata hivyo ametoa rai kwa Kamati hizo kujiandaa na tukio kubwa la kitaifa la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu na kuwasisitiza kuendelea kuhamasisha maandalizi ya msimu mpya wa kilimo sanjari na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya zao
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.