Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa mabilioni ya fedha kutekeleza Miradi mikubwa ya kitaifa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami nzito.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni Ujenzi wa barabara ya Mbinga Mbambabay kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 66 kwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 129..
Mradi mwingine ambao unaendelea kutekelezwa ameutaja kuwa ni Ujenzi wa barabara ya Amani Makoro - Ruanda (kilometa 35) kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi Bilioni 60.481 ambapo hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 24.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.