MAHAKAMA YAMTIA HATIANI KATIBU WA WENYE ULEMAVU LIPARAMBA
Mahakama ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imemhukumu Rainery Ngonyani adhabu ya *kulipa faini ya shilingi 100,000/- au kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la ubadhilifu.
Mshitakiwa alishtakiwa kwa kosa la ubadhilifu kinyume na Kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 mapitio ya 2022 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 mapitio ya 2022 kwa kujipatia manufaa ya shilingi milioni mbili, fedha za kikundi cha Wenye ulemavu Liparamba wilayani humo.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa fedha hizo kilipewa kikundi cha wenye ulemavu kutoka Akaunti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa kwa ajili ya kina mama,watoto na wenye ulemavu na hivyo kufanya upotevu wa kiasi hicho ambacho ni mali ya Halmashauri ya Nyasa.
Mshtakiwa amelipa faini.
Kesi hiyo ni ya Jamhuri dhidi ya Bw. Rainely Mathias Ngonyani ambaye ni katibu wa kikundi cha Walemavu Liparamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.
Kesi iliongozwa na Wakili Mwandamizi Mwinyi Yahaya ambapo mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kukiri kosa lake na kuthibitisha kuwa amesharejesha fedha 2,000,000/- kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.