• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MASHINE ya kisasa ya kuchakata mbao itakavyoongeza thamani ya mazao ya misitu Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: December 7th, 2020



SHIRIKA la kimataifa la WWF  limekiwezesha kijiji cha Sautimoja kilichopo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kununua mashine ya kisasa ili kuchakata mbao na kuongeza thamani ya mazao ya misitu.

Mtaalam wa kuendesha mashine hiyo  kutoka Shirika la Mpingo (MCDI) Yusuf Kiangio akizungumza katika Kijiji cha Sautimoja  amesema   mashine hiyo ni kiwanda kidogo kwa kuwa imeweza kutoa ajira kwa vijana waliopo katika kijiji cha Sautimoja hivyo kutekeleza kwa vitendo lengo la serikali ya viwanda.

Amesema mashine hiyo imeongeza thamani ya mbao na faida kubwa imepatikana katika maeneo ambayo mashine hiyo imetumika Kilwa mkoani Lindi na Tunduru mkoani Ruvuma.Amesema mashine ya kuchakata mbao Kilwa imewezesha kijiji kupata milioni 126 ukilinganisha na mapato ya milioni 26 zilizopatikana kabla ya kutumia mashine hiyo.

“Kwa mashine inayotumika katika kijiji cha Sautimoja kwa magogo yenye meta za ujazo 125 kabla ya kutumia mashine hii huwa wanapata shilingi milioni 30,lakini baada ya kuuza mbao zenye ujazo huo kupitia mashine hii wamepata shilingi milioni 90’’,alisema.Kutokana na matokeo hayo mashine hiyo imekuwa na ufanisi mkubwa katika kuongeza  thamani ya mnyororo wa mazao ya misitu.

 Kwa upande wake Mratibu wa FORVAC Mkoa wa Ruvuma Marcel Mtunda akizungumza mbele ya waandishi wa habari baada ya kuona utendaji wa mashine hiyo,amesema mashine hiyo ya kuchakata magogo ni ya kisasa na inaweza kutembea kwenda hata msituni kuchaka magogo.

Amesema mashine hiyo ambayo imenunuliwa nchini Canada kwa shilingi milioni 70, inapochakata mbao,ubao unaotoka unakuwa na ubora wa hali ya juu ukilinganisha na mbao ambazo zimechakatwa na mashine nyingine.

“Mbao zilizochakatwa na mashine hii, zina soko kubwa na bei yake ni ya juu tofauti na mbao zilizochakatwa na mashine nyingine hali hiyo ndiyo imeifanya mashine hii kuwa na sifa tofauti ikiwemo kuzalisha mbao nyingi zenye ubora kwa haraka’’,alisema Mtunda.

Mtunda amesema program ya FORVAC katika Mkoa wa Ruvuma inafanyika katika wilaya tano ambazo ni Tunduru, Namtumbo, Songea,Mbinga na Nyasa na kwamba FORVAC imedhamiria Kuongeza faida za kiuchumi, kijamii na kimazingira kutokana na usimamizi endelevu wa raslimali za misitu

Kwa upande wake Mtaalam wa Misitu wa Mradi wa FORVAC Alex Njahani  amesema katika nchi nzima mradi huo unatekelezwa katika wilaya 11 zilizopo mikoa ya Tanga,Ruvuma,Lindi na Dodoma

Hata hivyo amesma hadi sasa mashine mbili tu kuchakata mbao  zimenunuliwa katika  mikoa ya Ruvuma na Lindi na kwamba lengo ni kuhakikisha kuwa mashine hizo zinatolewa katika maeneo yote ambayo yanatekeleza mradi wa kuvuna msitu.

Emanuel Msoffe ni Mratibu wa Taifa wa mradi wa FORVAC amesema ununuzi wa mashine hiyo ya kisasa  katika kijiji cha Sautimoja,umekidhi malengo ya FORVAC ya kuongeza thamani mazao ya misitu.

“Mashine zilizonunuliwa siku za nyuma zilikuwa na kiwango cha asilimia 30 cha kufikia ule ubora unaohitajika,lakini mashine hii imefikia kiwango cha asilimia 63,tunataka kwenda zaidi ya asilimia 80’’,alisisitiza Msoffe.

Kwa mujibu wa Msoffe,takwimu zinaonesha kuwa jumla ya hekta 469,000 za misitu zinapotea kwa mwaka ambapo amesema upoteaji huo pia unachangiwa na utumiaji wa mazao ya mistu usiokuwa sahihi hivyo mashine hiyo ni msaada mkubwa kulinda misitu.


Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Desemba 6,2020  

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.