Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe. Kisare Matiku Makori amewataka wataalamu wa Wilaya ya Mbinga kuzingatia vigezo vya mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 na vipengele vyake ili kuibuka kinara
Vigezo hivyo vyenye jumla ya alama 100 ni pamoja na ufanisi wa usimamiaji wa miradi ya maendeleo (alama 32), ufanisi katika mapokezi ya Mwenge alama 6), uzingatiaji wa itifaki za mwenge (alama 8) na umahiri katika uandishi, usomaji na uwasilishaji wa risala ya utii kwa Mheshimiwa Rais (alamai 8).
Vigezo vingine ni uraghibishaji wa falsafa ya mwenge kwa mwananchi (alama 4), uwezeshaji wa vijana (alama 20), uwezeshaji wa makundi yenye mahitaji maalumu na ukatili wa kijinsia (alamai 4) na juhudi zinazochukuliwa katika mapambano dhidi ya VVU/Ukimwi, dawa za kulevya na Malaria (alama 3).
Orodha ya vigezo pia inahusisha mapambano dhidi ya rushwa na changamoto za lishe duni (alama5) na ushiriki katika uhifadhi wa mazingira na uchaguzi wa serikali za mitaa (alama 10).
Mkuu wa Wilaya amesisitiza Wakati wa maandalizi ya kupokea Mwenge wa Uhuru inatakiwa kuzingatia vigezo vyote ili kuibuka vinara katika mbio za Mwengeya mwaka huu.
Mwenge wa Uhuru unatarajia kuanza mbio zake mkoani Ruvuma Juni 8 mwaka huu
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.