Mbunge wa Jimbo la Nyasa, mkoani Ruvuma, Mhandisi Stella Manyanya, ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Nyasa iliyopo Nangombo kwa ziara ya kikazi na kukagua ujenzi wa jengo la jiko linalojengwa hospitalini hapo.
Jengo hilo linalenga kusaidia wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kuandaa chakula katika mazingira salama.
Kwa mujibu wa Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo, Bw. Maltin Ngole, ujenzi wa jiko hilo unafadhiliwa na Mfuko wa Jimbo kwa gharama ya Shilingi milioni tano, ambazo pia zilitumika kusawazisha eneo la hospitali.
Ujenzi huo uko katika hatua ya umaliziaji, na kukamilika kwake kutasaidia kuondoa changamoto ya wagonjwa kupikia nje.
Wananchi waliokuwepo hospitalini hapo wameeleza kufurahishwa na juhudi za Mbunge Manyanya katika kutatua changamoto hiyo, hasa kipindi hiki cha mvua, ambapo wagonjwa walikuwa na shida ya kupikia nje.
Wameeleza kuwa hatua hiyo itaongeza ustawi wa wagonjwa na kuboresha huduma hospitalini hapo.
Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Mbunge Manyanya za kuboresha huduma za kijamii wilayani Nyasa, ambapo amekuwa mstari wa mbele kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuboresha maisha ya wananchi wa jimbo hilo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.