SERIKALI kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF imetoa Zaidi ya shilingi milioni 395 kujenga miradi 6 katika vijiji vya Parangu na Mdunduwalo vilivyopo Songea Vijijini
Hayo yamesemwa na Katibu tawala Wilaya ya Songea Pendo Daniel kwenye mkutano uliofanyika kata ya Maposeni akieleza namna Serikali ilivyo amua kutekeleza miradi miwili ya maendeleo katika vijiji hivyo kwani lengo la Serikali kuishirikisha jamii dhana ya kujitegemea
Akizungumza kwenye mkutano huo mbele ya uongozi wa halmashauri pamoja na Wananchi, alisema kukamilika kwa miradi hiyo italeta tija kwao kwani wataweza kufanya biashara za uhakika pia ni jukumu lao kushiriki hatua zote za ujenzi wa miradi hiyo
“Ni matumaini yangu miradi hii itakuza uchumi wa kaya pamoja na kuongezeka kwa kipato cha mtu mmoja mmoja pia kujengwa kwa miradi hii 6 katika vijiji vya Parangu na Mdunduwalo itaongeza upatikanaji wa uduma mbalimbali za kijamii”alisema Pendo Daniel
Hata hivyo amewasisitiza viongozi wa vijiji pamoja na kamati za ujenzi wa miradi hiyo kushirikiana na wananchi katika kutekeleza ujenzi kwani asilimia 10 ya ujenzi itatolewa na wananchi katika kufanikisha kukamlikia kwa miradi yote
Akizungumza mbele ya wananchi mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mhe, Menasi Komba amemshukuru Rias kwa kuwezesha kutoa fedha hizo za miradi kwani nifuraha kwao kujengewa miradi hiyo pia vile vile amewaomba wananchi wailinde mradi yote nakushiriki hatua zote za ujenzi
“Wale wote watakaobainika kuiba vifaa vya ujenzi kwenye miradi hii hatua zitachukuliwa pia niwaombe wajumbe na wanakamati wa miradi wa vijiji vyote viwili msishawishike hizi fedha zimeletwa kwa malengo kukuza uchumu wa kaya zetu”alisema Komba.
Naye Nicodemus Nyoni mwananchi wa kijiji cha Parangu amemshukuru Mbunge wa jimbo hilo Jesinita Mhagama kwa kuweza kupelekewa fedha za miradi wa ujenzi wa standi alisema kukamilika kwakwe kwao itawasaidia kujipatia kipato na itaongeza uhakika wa huduma mbalimbali
Fedha hizo ambazo zimetolewa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF ambapo kijiji cha Parangu kimepokea shilingi milioni 225 za ujenzi wa miradi mitatu ambapo ni standi, uwekaji wa vigaya pamoja na kujenga matundu manne ya vyoo na uzio
Vile vile kjiji cha Mdunduwalo kimopokea shilingi milioni 170 za ujenzi wa miradi mitatu ujenzi wa nyumba ya madaktari wa wili, matundu sita ya vyoo pamoja na uchimbaji wa kisima kirefu cha maji
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.