• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKUCHIKA amwaklisha Rais Magufuli ufunguzi Ofisi ya TAKUKURU Namtumbo

Imewekwa kuanzia tarehe: August 20th, 2020

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu Gorge Mkuchika amemwakilisha Rais Magufuli katika ufunguzi wa jengo la ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Namtumbo lililogharimu zaidi ya shilingi milioni 139.

Akizungumza kabla ya kufungua jengo hilo katika hafla iliyofanyika mjini Namtumbo Waziri Mkuchika amesema Rais Dkt.John Magufuli amemteua kufungua jengo hilo kwa niaba yake na kwamba Rais ameweka utaratibu wa kuyafungua majengo mapya ya TAKUKURU kwa nyakati tofauti na wasaidizi wake.

Ameagiza majengo mapya saba ya TAKUKURU ngazi ya wilaya yatumike vema katika mapambano dhidi ya rushwa pamoja na kuwafichua wala rushwa sanjari na kuacha kushiriki katika vitendo vya rushwa.

“Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Jemedari Rais wetu,imefanya kazi kubwa ya kuimarisha na kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini’’,alisisitiza Waziri Mkuchika.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika,ripoti ya Benki ya Dunia ya Septemba 26,2019,imeeleza kuwa Tanzania imeongoza kwa kupunguza umaskini miongoni mwa nchi za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kulingana na Waziri Mkuchika,ripoti nyingine ya Benki ya Dunia inayoitwa Human Capital,The Real Wealth Of Nationals iliyotoka Julai 2019 ilionesha kuwa umasikini nchini Tanzania umepungua kutoka asilimia 34.4 hadi kufikia asilimia 26.8.

Waziri Mkuchika amesema ufanisi wa jitihada za serikali katika mapambano dhidi ya rushwa nchini katika mwaka 2018/2019 zimeendelea kuonesha pia kupitia taarifa za utafiti wa kupima hali  ya rushwa duniani unaofanywa  na wadau wa mapambano dhidi ya rushwa na utawala bora kama Taasisi ya Transparency International, MO Ibrahim na Afro Barometer.

“Taarifa za Taasisi hizo zote kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 zinaonesha kuwa Tanzania imeendelea kufanya vyema katika mapambano dhidi ya Rushwa’’,alisisitiza Mkuchika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU aliyewakilishwa na Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa wa TAKUKURU Sabina Seja amesema jengo hilo ni moja kati ya majengo mapya saba ya TAKUKURU ngazi ya Wilaya yaliojengwa kwa wakati mmoja.

Seja amesema TAKUKURU katika Mkoa wa Ruvuma hadi kufikia Juni 2020 imefanikiwa kuchunguza ubadhirifu na kuokoa  kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 740.

‘Fedha hizo zimeweza kuokolewa kutokana na uchunguzi katika  Benki ya wananchi wa Mbinga,vyama vya ushirika na kuwezesha baadhi ya watuhumiwa kurejesha fedha,vitendo hivyo vya ubadhirifu vilikuwa vinadumaza maendeleo ya ushirika nchini’’,alisema Seja.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza katika hafla hiyo amewaasa TAKUKURU kuendelea kuwang’ata wala rushwa na mafisadi wote bila kuwaonea na kuwapendelea ili kutomekeza rushwa nchini.

Mndeme amesema jengo hilo la TAKUKURU wilaya ya Namtumbo litaimarisha utendaji kazi wa watumishi wa TAKUKURU na kurahisisha watoa taarifa na mashahidi watakaoletwa katika opereshani mbalimbali za mapambano ya rushwa na kufanya kazi kwa uhuru na usiri zaidi.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Agosti 20,2020

Namtumbo

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.