• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKUU wa Mkoa aagiza raia ambao sio watanzania kudhibitiwa

Imewekwa kuanzia tarehe: March 4th, 2020

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme,amemtaka wakala wa usajili ufilisi na udhamini(RITA)na wakuu wa wilaya zinazopakana na Nchi jirani kuhakikisha wanawadhibiti watoto walio na umri chini ya miaka mitano ambao sio raia wa Tanzania kuingizwa kwenye mpango wa usajili wa vizazi utakaoanza mapema mwaka huu.

Mndeme alitoa rai hiyo jana wakati alipokuwa akifungua warsha ya viongozi wa wilaya na mkoa wa Ruvuma kuhusu usajili wa vizazi kwa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa manispaa ya Songea mkoani humo.

Alisema kuna baadhi ya wilaya mkoani humo zinapakana na Nchi jirani za Msumbiji na Malawi hivyo katika kukabiliana na changamoto hiyo ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha  watoto hao wasio na sifa hawasajiliwi katika mpango huo na kwamba watakaosajiliwa ni wale waliokidhi vigezo.

Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Ruvuma Mndeme,amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawasajili watoto wao pindi wanapozaliwa kwa lengo la kuiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi ili iweze kupanga mipango ya maendeleo ya muda mfupi na mrefu kwa madai kwamba bila ya kufanya hivyo itakuwa vigumu kuweza kujua mahitaji halisi kwa ya wananchi.

“Nawaombeni wasajili kwenye vituo vya tiba na watendaji wa kata mtangulize uzalendo na uadilifu katika mpango huo kwa lengo la kuepuka urasimu utakaosababisha wananchi kutozwa fedha hivyo yeyote atakayekwenda kinyume na utaratibu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sharia”Alisema Mndeme

Hata hivyo Mndeme ameonyesha kutoridhishwa na takwimu za sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 ambayo inaonesha ni asilimia 6 pekee ya watoto wa mkoa wa Ruvuma ndio waliosajiliwa nakupatiwa vyeti vya kuzaliwa  ambapo amedai kwamba kwa ujumla takwimu hizo hazirizishi na haziwezi kusaidia kupanga mipango ya maendeleo.

Awali kaimu Afisa mtendaji mkuu wa RITA Emmy Hudson alisema kuwa lengo la warsha hiyo ni kutoa hamasa kwa ajili ya usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano kwa madai kwamba mpaka sasa kiwango cha watoto waliosajiliwa ni kidogo.

Hudson aliongeza kusema kuwa mpaka sasa watoto walio na umri chini ya miaka mitano waliosajiliwa hapa Nchini ni zaidi ya milioni nne na kwamba katika kuboresha mpango huo wameamua kusogeza huduma hiyo kwa lengo la kuwapunguzia adha yaufuatiliaji na kuwapunguzia gharama.

Kaimu Afisa mtendaji huyo mkuu wa RITA Hudson aliendelea kusema kuwa katika kuboresha mpango huo,huduma zitakuwa zinapatikana katika ofisi zote za watendaji kata na vituo vya Tiba vinavyotoa huduma ya mama na mtoto.

Warsha hiyo imeshirikisha viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya,wenyeviti wa Halmashauri,wakurugenzi wa Halmashauri,makatibu tawala,makatibu tawala wasaidizi,viongozi wa Dini na wawakilishi wa wadau wa maendeleo wakiwemo UNICEF.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.