• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MTATIRO amtembelea mwalimu aliyejifungua watoto wanne Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: June 26th, 2022

MWALIMU wa shule ya msingi Wenje kata ya Nalasi wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Judith Chawe(29), amejifungua watoto wanne katika Hospitali ya Misheni Mbesa wilayani humo.

Mwalimu Judith alisema kuwa,watoto aliojifungua wenye jinsia ya kiume ni wawili na wa kike wawili na alifungua kwa njia ya kawaida na wanaendelea vizuri na kuongeza kuwa huo ni uzazi wake wa pili.

“kwanza namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kujifungua salama,lakini kutokana na mahitaji makubwa ya watoto wangu  nawaomba wasamaria wema na Watanzania wenzangu wenye mapenzi mema wanisaidie  mahitaji mbalimbali kama fedha na maziwa ili niweze kuwalea  hawa watoto”alisema Mwalimu Chawe.

Alisema,wakati anahudhuria kliniki Madaktari walimweleza kuwa ana watoto watatu tumboni,lakini kumbe walikuwa wanne  na kumshukuru Mungu kwa kumwezesha kupata watoto  hao na ameruhusiwa kurudi nyumbani.

Baba mzazi wa watoto hao Hamis Shaibu amemshukuru Mungu kwa kumwezesha kupata watoto wanne kwa mkupuo,hata hivyo ameiomba jamii iweze kuwasaidia  kwa hali na mali  mahitaji ya watoto hao.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amefika nyumbani kwa Mwalimu huyo ili kumjulia hali  na kuwaona watoto hao ambapo amewaomba Watanzania wenye mapenzi mema kumsaidia Mwalimu Judith ili aweze kuhudumia watoto hao wanaohitaji  gharama kubwa.

Mtatiro alisema,watoto hao wanahitaji msaada na huduma ya karibu kwa sababu maziwa ya mama peke yake hayatoshelezi kuwahudumia watoto hao wote wanne.

Alisema,serikali itakuwa bega kwa bega na Mwalimu huyo ili kuona maendeleo ya afya yake na watoto hao na amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Tunduru Ombeni Hingi, kuhakikisha Halmashauri inampatia gari Mwalimu huyo kila atakapohitaji  kwenda Hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa afya ya Mwalimu huyo na watoto wake.

Alisema,kazi ya malezi ya watoto wanne ni kubwa kwa hiyo lazima Serikali na jamii kumsaidia Mwalimu Judith katika malezi ya watoto hao waendelee kukua vizuri na kuwa na afya njema.

Awali Afisa Tarafa wa Nalasi  Salum Kijumu alisema, baada ya kupata taarifa ya Mwalimu Judith kujifungua watoto wanne wameanza utaratibu wa kumchangia  fedha kutoka kwa watumishi wanaofanya kazi katika Tarafa hiyo ili ziweze kusaidia mahitaji ya watoto hao.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MSIKIMBILIE hasara,serikali inakuja na bei ya neema kwa mahindi Julai

    May 31, 2025
  • WAKULIMA Namtumbo wachuma neema ya ufuta kwa teknlojia mpya ya mnada wa kidigitali

    May 31, 2025
  • RUSHWA yazidi kuporomoka na kukosa nafasi Ruvuma

    May 31, 2025
  • SERIKALI yatoa fidia ya bilioni 2.5 kupisha mradi wa umeme wa Grid Songea-Tunduru

    May 31, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.