Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mheshimiwa Humphrey Polepole amefanya ziara mkoani Ruvuma katika Wilaya ya Nyasa, lengo likiwa kutazama fursa zilizopo katika ushoroba wa Mtwara hadi bandari Ndumbi.
Balozi Polepole amesema ziara yake mkoani umo ni kuendelea kuitafutia nchi fursa mbalimbali kutoka nje ya nchi ambazo zitakuwa na manufaa kwa wananchi pamoja na serikali, uku akiwataka wadau mbalimbali kuchangamkia fursa katika ushoroba wa Mtwara.
Hata hivyo ameeleza kuwa ushoroba huo ni mfupi Zaidi kunisi mwa nchi za Afrika kuliko shoroba zote, kwani barabara yake inayo jumla ya umbali wa kilomita 822 kutoka bandari ya Mtwara mpaka bandari ya Ndumbi.
“Kazi yetu sisi tuliopewa dhamana ya kuiwakilisha nchi uko nje ni kutafuta fursa zitakazo ongeza mapato kwa taifa, nimetoa ombi kwa mkuu wa mkoa, tunaanzishe eneo la kiuchumi ambalo bidhaa zote zinazopatikana kariakoo zipatikane hapa ili kuwavuta wafanya biashara wa nchii jirani Malawi na msumbiji” alisema Polepole.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas, ameishukuru serikali kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa bandari ya ndumbi ambayo imegarimu Zaidi ya bilioni 12, alisema hii ni faraja kwa mkoa na kwa wilaya ya nyasa
“Kama Mkoa, sisi tumeshajianda tayari kuanzia maeneo maalum ya uwekezaji ambapo bidhaa zote zinazohitajika nchi jirani tulizopakana nazo Malawi na Msumbiji, kuwa bidhaa hizo zitapatikana hapa na lengo nikupunguza umbali wa wao kwenda dar es salaam na kama mkoa tupo tayari kuwawezesha wafanya biashara” alisema Kanali Thomas
Hata hivyo kwasasa mradi huo umekamlika na upo hatua ya uangalizi wa mwaka mmoja na upo tayari kwa matumizi, kukamilika kwa mradi huo itarahisisha Wilaya ya Nyasa kuinuka kwa uchumi
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.