• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

NYASA yaidhinishiwa bilioni kumi kutekeleza shughuli za maendeleo

Imewekwa kuanzia tarehe: November 5th, 2023

SERIKALI imeidhinisha zaidi ya shilingi bilioni kumi kwa ajili ya kutekeleza shughuli za mendeleo katika Halmashauri ya Nyasa mkoani Ruvuma  katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa Ndugu Khalid Khalif  wakati anazungumza na wanahabari ofisini kwake Kilosa mjini Mbambabay.

Amesema kati ya fedha hizo zaidi ya shilingi bilioni 4.1 ni fedha za ndani na zaidi ya shilngi bilioni 5.9 ni fedha za nje  na kwamba kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri hiyo imepokea zaidi ya shilingi bilioni 7.9 sawa na asilimia 78.6  ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 3.3 fedha za ndani.

“Halmashauri pia imepokea zaidi ya shilingi bilioni 4.5  fedha za nje  na  zaidi ya shilingi milioni 319,fedha zilizotolewa nje ya bajeti  hivyo kufanya mapokezi ya fedha zote kuwa ni zaidi ya shilingi bilioni 8.2’’,alisema Khalif.

Hata hivyo amesema hadi kufikia Juni 30 mwaka huu zaidi ya shilingi bilioni 6.6 zilikuwa zimetumika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo sawa na asilimia 80 ya fedha zilizopokelewa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyasa Mheshimiwa Sterwat Nombo  amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 2.9 kutekeleza mradi wa jengo la ofisi ya Mkrugenzi wa Halmashauri ya Nyasa ambapo hivi sasa watalaam wanafanya kazi vizuri ya kuwahudumia wananchi.

Amesema serikali hadi sasa imetoa shilingi bilioni 3.3 kuboresha miundombinu ya afya katika hospitali ya wilaya ya Nyasa ambapo hivi sasa wananchi wanapata huduma zote muhimu ndani ya wilaya.

Amesisitiza kuwa miaka mitatu ya Rais Samia imeleta faraja kubwa kwa wananchi wa Nyasa na kwamba kumekuwa na mafuriko ya miradi ya mabilioni ya fedha iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa  katika Halmashauri hiyo.

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ni miongoni mwa Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma ambayo inapakana na nchi za Malawi na Msumbiji.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.