• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

OPARESHENI ya kuwaondoa wafugaji maeneo wasiostahili kuanza Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: November 12th, 2022

Oparesheni ya kuwaondoa wafugaji katika maeneo wasiostahili kuanza mkoani Ruvuma

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameagiza wafugaji wote ambao wameingiza mifugo yao kwenye maeneo wasiostahili warudi kwenye maeneo yao ya vitalu.

Ametoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara wakati anasuluhisha mgogoro wa wakulima na wafugaji wa Kijiji cha Mkongo wilayani Namtumbo uliosababisha watu wanne kupoteza Maisha.

Mkuu wa Mkoa ameagiza wafugaji wote waliongiza mifugo yao bila vibali,wapeleke mifugo yao katika maeneo yenye vitalu vya wafugaji ambapo katika Mkoa wa Ruvuma wilaya ya Tunduru  ina vitalu vya kutosha kwa ajili ya wafugaji.

“Mkoa wa Ruvuma ndiyo Mkoa pekee nchini ambao umetenga vitalu kwa ajili ya wafugaji,Katika wilaya ya Tunduru kitalu kimoja kina hekari 500,hadi sasa kuna vitalu 107 ambavyo vipo wazi kwa ajili ya wafugaji’’,alisisitiza.

RC Thomas ametoa mwezi mmoja kwa wakuu wa wilaya zote kusimamia zoezi la utambuzi wa mifugo yote iliyopo kwenye maeneo yao kama ina vibali na namna vibali vilivyotolewa.

“Utoaji wa vibali vya mifugo hivi sasa umekuwa ni holela na kuna mazingira ya rushwa,kila mtu amekuwa anatoa vibali hali inayosababisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji’’,alisema Kanali Thomas.

Hata hivyo amesema kuanzia Novemba 10,2022 ni marufuku kuingiza mifugo mkoani Ruvuma hadi hapo uhakiki wa kubaini mifugo utakapokamilika.

Amesisitiza kuwa zoezi la utambuzi wa mifugo linaanza Novemba 10 na linatarajia kukamilika Desemba 9 mwaka huu na kwamba baada ya hapo oparesheni kabambe ya kuondoa mifugo iliyopo katika maeneo yasiyostahili itafanyika katika Mkoa mzima.

Mkuu wa Mkoa amewaagiza wakuu wa wilaya kuwachukulia hatua za kinidhamu wenyeviti wote wa vijiji na watendaji wanaohusika katika kuleta migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

Amemwagiza Mkuu wa TAKUKURU kuchunguza tuhuma dhidi ya wenyeviti wa vijiji ambao wanatuhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa wafugaji.

Kwa upande wake Awadhi Haji Kamishina wa Operasheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania akizungumza kwenye mkutano huo,amesema migogoro ya wakulima na wafugaji hivi sasa imeshamiri katika Kanda ya Kusini.

Amesema  migogoro hiyo inasababishwa na watu wachache waliopewa dhamana kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa sababu mbalimbali zikiwemo rushwa hivyo kuruhusu wafugaji kuingia katika maeneo ambayo hawastahili.

Amewataka wafugaji walioingia kinyume na taratibu kuondoka  na kwamba vitendo hivyo havitavumiliwa na matukio hayo yakijitokeza  tena jeshi la polisi litachukua hatua kali.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dkt.Julius Ningu amesema serikali hairidhiki na mifugo inayoingia kwenye mashamba ya wakulima na imekuwa inachukua hatua kukabiliana na hali hiyo.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Novemba 12,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.