MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina mndeme akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalma Mkoa wa Wilaya ya Songea amekagua mradi wa uwanja wa ndege wa Songea katika eneo la Ruhuwiko Manispaa ya Songea .
Uwanja huo ambao upo katika hatua za mwisho za umaliziaji unajengwa kwa serikali kwa gharama ya zaidi shilingi billioni 37 .Uwanja huo una urefu wa kilometa 1.8 na unajengwa na Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya CHICCO ya watu wa China .akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa, msimamizi wa ujenzi wa uwanja huo amemthibitishia Mkuu wa Mkoa kuwa ndani ya wiki inayoishia Oktoba 11 uwanja wa ndege wa Songea utakuwa umekamilika na kuanza kuruhusu kutua ndege kubwa aina ya Bombardier.
Uwanja wa ndege songea ni miongoni mwa viwanja vya Ndege vikubwa vinavyojengwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.Kukamilika kw uwanja huu kutafungua fursa utalii na uwekezaji katika Mkoa wa Ruvuma.
Imeandkiwa na Mawazo Mwaijengo
Oktoba 10,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.