SEKONDARI mpya ya wasichana ya Mkoa wa Ruvuma iliyosajiriwa kwa jina la Dkt Samia Suluhu Hassan imejengwa Wilaya ya Namtumbo inatarajia kuanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano Julai 2023.
Serikali ya Awamu ya Sita imetenga shilingi bilioni nne kupitia program ya kuboresha elimu ya sekondari nchini (SEQUIP) kutekeleza mradi huu ambapo hadi sasa zimetumika shilingi bilioni tatu na kazi inaendelea.
Sekondari hii ikikamilika kwa asilimia 100 itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1000.
Serikali imetoa shilingi bilioni 7.7 katika Mkoa wa Ruvuma kupitia program ya SEQUIP kujenga sekondari mpya 11 katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma ikiwemo sekondari hii ya wasichana ya Mkoa wa Ruvuma iliyojengwa eneo la Migelegele Kata ya Rwinga Wilaya ya Namtumbo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.