Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amesema sekta binafsi ni taasisi zinazoweza kuchangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.
Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la Biashara Mkoa wa Ruvuma, kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Amesema mpango mkakati wa mkoa unapoandaliwa ni lazima uendane na ilani ya Chama cha Mapinduzi, vipaumbele vya Mheshimiwa Rais, makundi ya kidini na makundi mengine maalumu bila kuiacha sekta ya biashara au binafsi.
Amebainisha kuwa takwimu za mapato za mkoa wa Ruvuma kwa mwaka 2023 zinaonyesha kuwa pato la mkoa ni trilioni 7.17, uchangiaji kwenye pato la taifa ni asilimia 3.8 na kipato cha mtu mmoja mmoja ni milioni 3.75.
Ameeleza kuwa sekta ya kilimo inaongoza kutoa mchango mkubwa wa ukuaji wa uchumi wa mkoa na uchangiaji katika pato la taifa, ikufuatiwa na sekta ya madini na sekta zingine ikiwemo ya biashara.
Kanali Ahmed amesema kama mkoa ungeongeza thamani ya kile kinachozalishwa kwenye sekta ya kilimo basi mkoa ungekuwa na pato kubwa zaidi ya lililopo sasa kupitia sekta hiyo ya kilimo pekee.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amesema mkoa utaendelea kutoa ushirikiano kwa sekta binafsi kwa kuwa ni kichocheo cha uchumi.
Amesema wataendelea kushirikiana kutatua changamoto kubwa na ndogo na kufanya ubunifu ili kuhakikisha wanapata fursa zaidi kwa kuwa Ruvuma ni mkoa wa kimkakati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.