Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Damas Ndumbaro amesema Wizara yake imejipanga kubadilisha kazi za sanaa, utamaduni na michezo kuwa miongoni mwa bidhaa adimu.
Dkt. Ndumbaro amesema hayo wakati anazungumza kwenye tamasha la kabila la wamatengo lililofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mtama, kata ya Utiri Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma.
Dkt.Ndumbaro amesisitiza kuwa kazi za ubunifu zikiwekwa vizuri zitakuwa ni chanzo cha mapato na kukuza uchumi wa wasanii na Taifa kwa ujumla.
Amesisitiza kuwa Wizara yake inatarajia kufanya tamasha kubwa la utamaduni katika mkoa wa Ruvuma ambalo litafanyika mwakani kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
"Tumejipanga kuwatafutia soko kubwa la kimataifa wabunifu wanaosuka visonjo , vikapu na sanaa nyingine za mikono ili wafaidike na kazi wanazozifanya," alisema Mhe. Dkt. Ndumbaro.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.