• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI yaridhia wakulima Ruvuma kuendelea na mfumo wa stakabadhi ghalani

Imewekwa kuanzia tarehe: June 26th, 2023

IMkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeridhia wakulima kuendelea kuuza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Kanali Thomas amesemayo hayo mjini Tunduru wakati anazungumza na viongozi na watendaji wa Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma katika majumuisho ya vikao maalum vya mabaraza ya madiwani  ya kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  vilivyofanyika kila Halmashauri kuanzia Juni 19 hadi 26,2023.

“Kupitia kikao hiki napenda kuwajulisha kuwa Waziri wa Kilimo ameandika barua ya kuridhia mfumo wa stakabadhi ghalani kuendelea kutumika katika Mkoa wa Ruvuma kutokana na mafanikio makubwa yanayopatikana kwa wakulima na Halmashauri kutokana na kuuza mazao kupitia mfumo huo’’,alisisitiza Kanali Thomas.

Amesema wakulima mkoani Ruvuma wameweza kuingiza zaidi ya shilingi bilioni 87 baada ya kuuza mazao ya ufuta,soya,mbaazi,korosho na kahawa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani  katika kipindi cha mwaka 2022/2023

Hata hivyo amesema wanaopinga mfumo huo sio wakulima bali ni   watu wa kati wakiwemo wafanyabiashara na baadhi ya watumishi na  madiwani katika Halmashauri ya Tunduru  wanaotorosha mazao na Kwenda kuyauza nje ya mfumo wa stakabadhi ghalani nje ya Mkoa wa Ruvuma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Komredi Oddo Mwisho akizungumza kwenye kikao hicho ameutaja mfumo wa stakabadhi ghalani kuwa upo kwenye Ilani ya CCM hivyo unatakiwa kutumika kuuza mazao ya wakulima ili kutoa tija baada ya wakulima kuuza mazao bei ya ushindani.

“Mfumo wa stakabadhi ghalani ni matakwa ya Ilani ya CCM,kipengele cha 34(i) kinazungumzia wakulima kuuza mazao ya stakabadhi ghalani,pia umetolewa mwongozo wa mazao yanayotakiwa kuuzwa kwenye mfumo huu”,amesisitiza Komred Mwisho.

Amesisitiza kuwa wakulima kuendelea kuuza mazao yao kupitia mfumo huo ni kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo hivyo wakulima  kufaidika badala ya kunyonywa na mfumo holela.

Amewatahadharisha wasiruhusiwe wafanyabiashara au mtu yeyote anayetaka kukwamisha mfumo wa stakabadhi ghalani ambao ni wa wakulima pekee.

Amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Ilani ya CCM ya mwaka 2020 hadi 2025 itahakikisha inasimamia mfumo wa stakabadhi ghalani na kutafuta masoko bora ya wakulima.

Mrajisi Msaidizi wa Ushirika Mkoa wa Ruvuma Peja Muhoja amezitaja faida za  Mfumo wa stakabadhi ghalani kuwa ni Pamoja na wakulima kukutanishwa na wanunuzi hivyo kuwafanya wawe na maamuzi ya kuuza mazao yao kwa umoja wao na kuwepo kwa matumizi ya vipimo halali vya wakulima kwa sababu wanunuzi hutumia mizani iliyohakikiwa na wakala wa vipimo.

Amezitaja faida nyingine za mfumo huo kuwa ni upatikanaji wa tozo za serikali kwa njia rahisi,kuongezeka kwa bei ya mazao ya ufuta,soya na mbaazi ambao umetokana na kuongezeka kwa wanunuzi ambao wanashindanishwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani na kutoa bei kubwa kwa wakulima.

Mwisho

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.