SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi milioni 500 kujenga wodi mbili za upasuaji katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea iliyojengwa kwenye kijiji cha Mpitimbi Songea.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Neema Maghembe wakati anatoa taarifa ya mradi huo kwa Timu ya Menejimenti Mkoa iliyoongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki.
Maghembe amesema fedha hizo pia zimetumika kujenga nyumba ya mochwari na kichomea taka na kwamba serikali pia imetoa shilingi milioni 68 kupitia TASAF kujenga nyumba ya mtumishi wa hospitali hiyo.
Hadi sasa serikali imejenga majengo 13 kati ya 24 yanayotakiwa katika hospitali hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.