• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SONGEA ilivyodhamiria wanafunzi wote waliofaulu kidato cha kwanza kuripoti shuleni

Imewekwa kuanzia tarehe: February 7th, 2024

Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma  Mheshimiwa Simon Kapinga amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kuwahamasisha Wazazi  na walezi kuhakikisha Watoto wote wanaostahili wanakwenda shuleni.

Kapinga ameyasema hayo wakati anazungumza kwenye Kikao cha robo ya pili cha Baraza la Madiwani  la Halmashauri hiyo kilichofanyika Lundusi mji mdogo wa Peramiho wilayani Songea.

“ kuna wanafunzi wamefaulu masomo yao ya kujiunga na kidato cha kwanza lakini  mpaka sasa hawajaripoti mashuleni,madiwani wenzangu tushirikiane na  watendaji wa kata,vijiji na wazazi kuhakikisha Watoto wote wanaripoti shuleni”,alisisitiza Kapinga. 


Mwenyekiti huyo pia amekemea tabia ya baadhi ya  wananchi wenye mashamba kuwatumikisha Watoto kwenye ajira mashambani hali ambayo inaathiri  ratiba za masomo yao ambapo ametaka tabia hiyo iachwe mara moja.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Neema Maghembe amesema ofisi yake  kupitia Idara za Elimu Msingi na Sekondari inaendelea kusimamia mahudhurio ya wanafunzi wa awali,msingi na sekondari ili kuhakikisha wanafunzi wote walioandikishwa na waliopangiwa kidato cha kwanza wanaripoti kwa asilimia 100.

Amesema hadi kufikia Januari 31 mwaka huu wanafunzi wa awali katika shule za Halmashauri hiyo walikuwa wameripoti kwa asilimia 99,darasa la kwanza asilimia 99 na wanafunzi wa kidato cha kwanza  wameripoti kwa asilimia 81.2

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amewapongeza  watumishi na wataalam  wakiwemo wakuu wa divisheni na vitengo katika Halmashauri hiyo, kwa kazi nzuri ambazo wamekuwa wakifanya, huku akisisitiza kuendelea kuchapa kazi kwa tija na ufanisi.

Halmashauri ya wilaya ya Songe ani miongoni mwa  Halmashauri nane zinazounda Mkoa wa Ruvuma

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.